Ratiba na vipindi vyetu, RocTV
NJE YA ULINGO | SAA 3:00 USIKU
Maelezo:
Kipindi maalum cha mahojiano (interview programme) kinachotoa fursa kwa muimbaji au mtu yeyote mwenye ushawishi wa kushirikisha watu kuhusu anachokifanya hata kama ni tofauti na watu wengi wanachokifahamu kutoka kwake. Lengo nikuleta uelewa kwa watu wajue kuwa wamezungukwa na fursa mbali mbali sio lazima kuegemea kwenye eneo moja tu.
SOUL FOOD | SAA 3:30 USIKU
Maelezo:
Hapa tunapata neno la faraja na kutia moyo (Word of Encouragement) kwakuzingatia andiko kutoka katika kitabu cha
Timotheo 3:16-17 “kila andiko lenye pumzi ya Mungu la faa kwa mafundisho”.
Hivyo kpindi hiki kina toa chakula cha rohoni ambachomkina leta afya ya kiroho (Soul food).
JIKONI LEO | SAA 12:00 JIONI
Maelezo:
Kipindi ambacho kina fundisha aina mbali mbali za mapishi na kushauri namna bora ya kuchagua chakula kwa kuzingatia afya ya mlaji, ili kupunguza magonjwa yatokanayo na mpangilio mbaya wa kula au ufanisi mdogo wa mapishi.
UMLEAVYO | SAA 3:00 USIKU
Maelezo:
Ni kipindi ambacho kinatambua umuhimu wa malezi ya watoto kama msingi mkuu kwenye maendeleo na ustawi wa jamii yoyote ile, hivyo kinazugumzia malezi ya watoto kuanzia wakiwa mimba mpaka wanapofika umri wa kuitwa watu wazima.
Hakuna vipindi kwa sasa..
GARI LAKO | SAA 3:00 USIKU
Maelezo:
Kipindi kinacho kupatia historia, ubora, faida na hasara zitokanazo machaguo ya aina za baadhi ya magari na kutoa mapendekezo ya ununuzi kulingana na uwezo wa mtu husika kiuchumi.
ROC SPORTS | SAA 1:00 USIKU
Maelezo:
Hapa tunaangazia masuala mbali mbali ya michezo ya ndani na nje ya nchi, hapa unapata taarifa za michezo ya aina zote bila kusahau uchambuzi wakina kutoka kwa watu wenye uweledi na masuala ya kimichezo.
HOW WE MET | SAA 3:00 USIKU
Maelezo:
Kipindi ambacho kina tambua umuhim wa mahusiano katika ustawi wa jamii yenye malengo ya kimaendeleo, hivyo mtazamaji anapata nafasi yakujua mambo mabali mbali ya kimahusiano. Mfano mahusiano ya Baba na mtoto wake wa kike, mama na mtoto wa kiume, Kaka na Dada, Mke na Mume, Kiongozi na wanao ongozwa, Muajiri na muajiriwa, pamoja na wapenzi ambao bado hawajaingia kwenye ndoa, lengo nikujua,changamoto,na kuleta uelewa juu ya nini kifanyike kua na mahusiano mzuri kama uti wa mgongo wa maendeleo.
TEN GOSPEL CUTS | SAA 12:00 JIONI
Kipindi hiki kinatoa fursa ya kufahamu ni nyimbo gani ambayo imefanya vizuri sana katika wiki husika. Kwa kuangalia ubora wa utunzi, watazamaji, muziki,video ubora wa audio namengine mengi amabyo yataifanya nyimbo kua na vigezo Zaidi ya nyingine, lengo nikuwapa moyo na motisha waimbaji kufanya kazi nzuri zaidi.
SCREENSHOT | SAA 1:00 USIKU
Maelezo:
Nikipindi ambacho kina toa habari zilizo jiri wiki zima hasa zile zilizo shika vichwa vya habari kwa wiki husika, lengo lakipindi hiki nikuwapa nafasi watu waliokosa muda wakutazama habari kutokana na kubanwa na shuguli za hapa na pale, tunaishi kwenye uli mwengu wa taarifa ambapo kula mtu anahaki yakupata habari ilikujua nini kinaendelea duniani.
SAUTI THERAPY | SAA 3:00 USIKU
Maelezo:
Ni kipindi kinachotoa nafasi kwa mtumishi wa MUNGU:- awe Muimbaji, Mpigaji, au Muhubiri kutoa huduma ya kiibada kwa watazamaji ambao wapo studio na wanao tazama kwenye runinga. Pia kusifu na kuabudu kunasimama kama lengo kubwa la kipindi hiki ili kubadilisha maisha ya watu ya kiroho na kimwili, kwasababu kipindi kina simama kama tiba kwa njia ya muziki (sauti therapy).
