Siku 5 za Kufunga na Kuomba

SIKU 5 ZA KUFUNGA NA KUOMBA

Isaya 55:11

Tunamshukuru sana Mungu kwa ajili ya neema hii aliyotupa kwa mara nyingine tena ya kuwa na mfungo huu, ni wakati wa kumshukuru Mungu kwa ajili ya mwezi huu na kujikabidhi kwake kwa ajili ya mwezi ujao.

Tutakuwa na prayer points zifuatazo;

  1. Mungu asante kwa neema na kibali cha kufunga na kuleta maombi yetu mbele zako.
  2. Ee Bwana, naomba neno ulilotupa na kila neno utakalotupa kupitia madhabahu yako likalete matunda kwenye maisha yangu katika kila mwezi uliotupa ndani ya huu mwaka.
  3. Mungu naomba udhihirisho wa mapenzi yako kwenye kila ninachokifanya ndani ya huu mwaka.
  4. Mungu nisaidie nilinde imani yangu kwenye neno lako, ili neno lako lifanikishe kusudi lako kwenye maisha yangu.

Jioni kuanzia saa kumi na moja tutakutana hapa kanisani Reality of Christ, Sinza Mori karibu kabisa na ofisi za TAMWA kwa ajili ya maombi ya pamoja. Vilevile tutakuwa Live kupitia ukurasa wetu wa YouTube https://www.youtube.com/@realityofchristchurch na kupitia ROC TV, King’amuzi cha Startimes Antenna, channel number 451.
Karibu sana.