KATI YA ULIPO NA UNAPOTAKIWA KUWA, USIKOSE SEMINA ”FROM ZERO TO HERO” WIKI HII

Kati ya ulipo sasa na mahali unapopaswa kuwa, kuna jambo ambalo Mungu anataka kukufundisha ili uweze kusogea mbele.

Huo ndio ujumbe unaobebwa katika semina maalumu ya siku tatu inayokwenda kwa jina la “FROM ZERO TO HERO”, inayotarajiwa kufanyika kuanzia Jumatano, Agosti 12 hadi Ijumaa, Agosti 14, 2026, katika kanisa la Reality of Christ Church, Sinza Mori, jijini Dar es Salaam.

Semina hii itaongozwa na Mtumishi wa Mungu, Bishop Sunbella Kyando, ambapo washiriki watapata nafasi ya kujifunza na kutafakari namna ya kuvuka changamoto za maisha, kujenga mtazamo mpya na kusonga mbele kuelekea hatma waliyoikusudia.

Ujumbe wa semina hii unasisitiza kuwa, licha ya hali ambayo mtu anaweza kuwa nayo leo, historia ya jana haipaswi kuamua hatma ya kesho. Changamoto, kushindwa au mazingira ya maisha ya nyuma havipaswi kuwa sababu ya mtu kukata tamaa, kwa kuwa bado kuna nafasi ya mabadiliko na mwanzo mpya.

“Ulipo sasa hivi sio mwisho wa safari. Mungu bado anaweza kukutoa, kwa kuwa hakuna linalomshinda.”

Semina itaanza saa 11 jioni, watu wote wakialikwa kutoka maeneo mbalimbali kushiriki katika siku zote tatu za mafundisho na kupata maarifa yatakayoweza kuwasaidia katika safari yao ya maisha.

Kwa wale ambao hawataweza kufika katika eneo la tukio, semina hiyo pia itarushwa moja kwa moja mubashara kupitia ukurasa wa YouTube wa Reality of Christ Church pamoja na RocTV.

Wapendwa wote wanahimizwa kutokuja peke yao, bali kuwaalika ndugu, marafiki na watu wengine ili nao wapate fursa ya kushiriki katika mafundisho hayo yenye lengo la kuwasaidia kusonga kutoka walipo kuelekea hatua nyingine ya maisha.