Pesa bado zipo nyie fungeni tu magoli..

Pongezi za Muheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu hassani kwa @simbasctanzania na @yangasc
Leo hii Mh Samia suluhu Hassan, katika sherehe za maadhimisho ya miezi miwili ya uongozi wake wa awamu ya sita, ameongea na kusema kuhusu million 5, kwaajili ya kununua magoli ya Simba na yanga, kwa Kila goli Moja bado zipo
Ameyasema hayo Leo jijini dar es salaam katika semina iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa CCM (UWT).

“Niwapongeze wanangu wa @yangasc na @simbasctanzania kwa kuitumia vizuri nafasi niliyowapa ya Goli Moja million 5 wameitumia vizuri sana kwa hesabu nilizonazo nadhani yanga wameshalamba milioni 30 na simba Jana milioni 35 na nyuma nadhani walikula 5, kwahiyo niwapongeze kwa kuitumia vema fursa hii.