Kiongozi Mkuu wa Makanisa ya Roman Cathoric Duniani Papa Francisco Ameteua Makardinali wapya 21 kati yao Makardinali hao walioteuliwa Mmoja ni Kutoka hapa Nchini Tanzania, Ambaye ni Askofu mwandamizi wa Jimbo kuu la Tabora, Askofu Protase Rugambwa.
Uteuzi huu umefanyika huko Vatcan makao makuu ya Kanisa la RC ukihusisha makardinali wengine kutoka nchi mbali mbali kuliko enea kwa Kanisa la RC, na kwa Bara la Africa wamepatikana Makardinali Watatu nao ni Askofu Mkuu Stephen Ameyu Martin MULLA kutoka jimbo kuu la Sudani, Stephen Brislin kutoka Jimbo kuu la Cape Town Afrika Kusini na wa tatu ni Askofu mwandamizi Protase Rugambwa kutoka Jimbo kuu la Tabora. Kwa pamoja makardinali hawa watatu wanakamilisha Orodha ya Makardinali wapya 21 walioteuliwa na Papa Francisco Kiongozi Mkuu wa Kanisala RC.
Makardinali hawa walioteuliwa watasimikwa rasmi tarehe 30 Septemba 2023.
