Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Club ya Yangasc NABI, Usiku wa kuamkia Leo ametangazwa Rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Club ya As FAR Rabat ya Nchini Morocco. Amechukua kandarasi hii mara baada ya kufikia ukomo na iliyokuwa Club yake.
Hii imemaliza sintofahamu iliyokuwa imetokea, watu wengi walikuwa na maswali juu ya Kocha huyu aliyeipa mafanikio timu ya Yanga. Kwani kabla ya hapo alihusishwa na tetezi ya kujiunga na Club ya @kcfcofficial ya Afrika Kusini, lakini haikuwa hivyo, baada ya fumbo hilo kufumbuliwa kwa Club ya @kcfcofficial kumtambulisha Kocha wake Mpya ambaye alikuwa tofauti na matarajio ya watu wengi.
Na sasa Nabi amefunga mjadala wote kwa kumtambulishwa rasmi kuwa kocha wa As FAR Rabat.
Hii imekupa somo Gani kwa Soka la Tanzania?
