48 Wajeruhiwa vibaya Johannesburg

Mlipuko unaodhaniwa kuwa niwa Gesi ya Ardhini Afrika kusini, katika Mji wa Johannesburg Mtaa wa Bree umesababisha kifo cha Mtu mmoja na majeruhi 48 katika mlipuko mkubwa, mlipuko huo umetokea Jana July 19 majira ya Jioni.

Msemaji wa Polisi wa Eneo hilo CPFs Alexandra amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuomba watu wachukue tahadhari ikiwemo kutofika eneo hilo, ili kuruhusu huduma za Dharura, huku akisema mlipuko huo huenda umetokana na njia za Gesi chini ya Ardhi.

Tukio katika mtaa wa Bree bado linachukuliwa kuwa eneo hatarishi huduma za dharura zimesalia hapo na watu wanahamishwa inapobidi.